Wanafunzi wa Tanzania wasomao nchini Algeria wanaendelea kusubiria fedha yao waliyotumiwa na bodi ya mikopo kwa zaidi ya mwezi sasa.Hali hii imesababisha wanafunzi kuishi maisha magumu katika kipindi chote cha likizo ndefu ya summer iliyomalizika hivi karibuni.Mwaka mpya wa masomo ambao umeanza mapema mwezi umewaacha wanafunzi wa Kitanzania hapa Algeria wakikosa kabisa maandalizi mazuri ya kujiandaa kimasomo,na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wanafunzi wapya wanaonza kozi zao hivi karibuni katika vyuo mbalimbali hapa Algeria
Uongozi wa wanafunzi hao unajitahidi bila mafanikio kuushawisho ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa ambako posho hiyo imekwama kwa takribani mwezi sasa kutusaidia kutuleta posho hiyo katika utaratibu wa awali uluozoeleka lakini jitihada hizo zinaonekana kugonga mwamba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment